Naibu Katibu Mkuu Wizara Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahera amesema Wizara inashirikiana kikamilifu na Shirika linaloshughulika na Kampeni ya Elimu kwa Mtoto wa Kike (CAMFED) katika kuhakikisha Wanafunzi waliokatisha masomo wanapata fursa ya elimu na ujifunzaji kuwezesha kufikia malengo yao.
Dkt. Mahera amesema hayo Septemba 24, 2024 jijini Dodoma katika kikao kilichowakutanisha viongozi wa elimu kutoka Tanzania, Zimbabwe, Zambia na Malawi kujadili juu ya uendeshaji wa program ya Stadi za maisha inayoendeshwa na shirika hilo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. Atupele Mwambene amesema majadiliano katika mkutano huo yanaisaidia Serikali kuboresha mikakati katika utekelezaji wa mageuzi ya elimu yanayolenga kuwa na rasilimaliwatu mahiri na yenye ujuzi.
Mkurugenzi wa Miradi na Ushirikiano CAMFED Tanzania Bi. Anna Sawaki amesema program ya elimu ya stadi za maisha inalenga kuwawezesha wanafunzi kuendelea kujifunza kwa umahiri na kwamba mradi huo kwa sasa unatekekezwa katika mikoa 10 ambayo ni Singida, Mwanza, Tabora, Iringa, Dodoma,Tanga, Pwani, Morogoro, Shinyanga na Dar es Salaam.