Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ametoa wito kwa wadau wanaojadili Rasimu ya Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Teknolojia za Kijiditali katika Elimu pamoja na mambo mengi kujadili namna bora ya kuratibu na kufungamanisha juhudi za wadau mbalimbali katika eneo hio nchini.
Prof. Nombo ametoa wito huo Juni 24,2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa kujadili Rasimu ya Mkakati huo ambapo pia amewataka kuona namna ya kuweka mazingira yatakayovutia na kuhamasisha matumizi ya pamoja ya miundombinu ya Teknolojia za kidigiti, rasilimali watu na rasilimali nyingine