Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Februari 19, 2024 amewasili wilayani Korogwe mkoani Tanga kwa kufungua Mafunzo ya Kitaifa ya kuwajengea uwezo Walimu Wakuu wa Shule za Msingi kutoka Wilaya ya Korogwe Mji, Korogwe Vijijini na Lushoto wapatao 347, kuhusu Uongozi, Usimamizi wa Shule na Utawala Bora yanayofanyika katika Chuo cha Ualimu Korogwe.