Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo April 28, 2024 amekutana na Balozi wa Tanzania The Hague Nchini Uholanzi Mhe. Caroline Kitana Chipeta kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Elimu.
Prof. Nombo amemweleza Balozi huyo kuhusu hatua mbalimbali za utekelezaji wa mageuzi katika Elimu yanayolenga kuzalisha Wahitimu mahiri watakaoweza kushindana katika soko la ajira Kitaifa na Kimataifa.
Amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya Elimu katika ngazi mbalimbali ikiwemo Elimu ya Amali na kwamba inaendelea na utekelezaji wa ujenzi wa Vyuo vya Ufundi Stadi kila Wilaya ili kuwezesha ujuzi kwa Vijana tarajiwa.
Viongozi hao pia wamejadiliana namna ya kuongeza fursa mbalimbali za ufadhili wa masomo katika fani za Uhandisi, Sayansi, Teknolojia na Tehama pamoja na mikakati itakayosaidia kuimarisha mafunzo ya ufundi stadi Nchini.