Katibu mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amekutana na kuzungumza na kampuni ya Mastercard Foundation ikiwa ni kujadili na kubaini vipaumbele, changamoto, na mipango katika kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika elimu ya sekondari ikiwemo uendelezaji wa walimu.
Mastercard Foundation ni shirika la kutoa misaada la nchini Kanada na Iinafanya kazi na mashirika yenye maono kuendeleza elimu na ushirikishwaji wa kifedha ili kuwawezesha vijana barani Afrika na vijana wa nchini Kanada kupata kazi yenye heshima na inayoridhisha.