Chumba cha Kidigitali (Smart Class) cha Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) chaikosha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo



Kamati hiyo ilifika katika Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na taasisi hiyo kupitia bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023/24 iliyopitishwa na Bunge.



Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Aneth Komba ameiambia Kamati kuwa Smart Classes zinatumika kutoa mafunzo kwa walimu katika Mpango wa Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini.

Dkt. Komba ameongeza kuwa TET iko katika mazungumzo na kampuni ya simu za mikononi Airtel ili kuwezesha kuwa na mtandao usio wa kulipia (zero tarrif) ili iwe rahisi kwa watumiaji wa madarasa hayo kupata mtandao kwa urahisi.

Kamati hiyo ilipata fursa ya kushuhudia namna _Smart Class_ inavyofanya kazi kwa kuunganishwa madarasa ya walimu yaliyokuwa yakiendelea katika vituo vya Zanzibar, Njombe, Dodoma na Ikwiriri

Akizungumza baada ya kuona namna madarasa hayo yanavyofanya kazi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Husna Sekiboko ameipongeza Taasisi hiyo na kutaka kuangalia namna ya kuwezesha kuwa na mtandao imara
ili kuwezesha mafunzo kutolewa bila changamoto yeyote