Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa, amesema Serikali itaendelea kuimarisha nguvu kazi yenye ujuzi ili iweze kushindana katika soko la ajira la ndani na kimataifa.



Mhe. Majaliwa amesema hayo 11 Oktoba 2025 jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.



Amesema maendeleo ya taifa yanategemea watu walioelimika na wenye maadili, hivyo Serikali inaendelea kuwekeza katika elimu bora na mafunzo ya ujuzi kupitia programu za VET na TVET pamoja na ujenzi wa vyuo vya ufundi katika kila wilaya. Kupitia Mpango wa Taifa wa Maendeleo ya Ujuzi, Serikali pia inaendelea kuandaa wataalamu katika sekta za kilimo, viwanda, nishati, teknolojia na huduma ili kuongeza tija ya uzalishaji.



Aidha, Waziri Mkuu amezitaka taasisi za elimu, sekta binafsi na vijana kushirikiana katika kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na kuzitaka kampuni na waajiri kuongeza fursa za mafunzo ya vitendo kwa vijana.



Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, amesema Serikali inaendelea kuboresha mfumo wa mikopo ya elimu ya juu ili kuongeza uwiano na usawa kwa wanafunzi wote wenye sifa.



Naye Mwenyekiti wa Kigoda cha Mwalimu Nyerere, Prof. Alexander Makulilo, amesema kongamano hilo linaendeleza fikra za Mwalimu Nyerere kwa kuhamasisha maadili, uzalendo na ujenzi wa taifa lenye watu wenye ujuzi na mchango chanya katika maendeleo