Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo madarasa, kuweka vifaa, tunataka kuhakikisha uwepo wa mazingira rafiki ya watoto ya wa Kitanzania kupata Elimu bila kikwazo.
Waziri Mkenda ametoa kauli hiyo Novemba 30, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika sherehe za Ufunguzi wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA)