
Wanafunzi katika Shule ya Msingi Azimio iliyopo Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe, wamefurahia ujenzi wa miundombinu bora na jumuishi inayotoa fursa ya elimu kwa wote ikiwemo wanafunzi wenye mahitaji Maalum.
Hawa Njovi, mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo ana malengo ya kuwa daktari wa watoto, amesema miundombinu rafiki inahamasisha ujifunzaji hivyo amewashauri wanafunzi wenye mahitaji Maalum wasikate tamaa.
Brian Bundala Mwanafunzi katika Shule hiyo amesema madarasa ya zamani hayakuwa salama, lakini miundombinu mipya inawapa hali ya kujiamini zaidi wawapo shuleni.
Naye, Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Maisha Mhapa ameeleza kuwa BOOST imewezesha ujenzi wa madarasa 9, ikiwemo madara mawili ya Elimu ya Awali, matunda ya vyoo 18 Kwa gharama ya Sh. Milioni 347.5
Mkazi wa Kata ya Mwembetogwa Mji wa Makambako Bw. Spear Sanga amesema miundombinu bora imewafanya wazazi wengi kuwahamishia watoto wao katika shule hiyo, na amesihukuru Serikali kwa utekelezaji wa mradi huo kwa mafanikio.