Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameipongeza Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) iliyomaliza muda kwa kufanya kazi ya kuishauri wizara juu ya usimamizi na uendeshaji wa Wakala kwa kuzingatia malengo yakekatika kutekeleza majukumu.
Prof. Nombo amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Bodi mpya ya Ushauri ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) ambapo ameongeza kuwa Kufuatia ushauri imesaidia kupitisha mipango mbalimbali ya Wakala inayohusu usimamzi wa fedha, usimamizi wa rasilimali watu, na mipango mingine ya utendaji wa Wakala.
"Usimamizi mzuri wa Bodi umesaidia Wakala kumefanikiwa kupata Hati safi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali - CAG, niwapongeze sana". Amesema Katibu Mkuu.
Prof. Nombo amesema Bodi hiyo mpya ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Wakala, kupitisha mipango ya Wakala,kuishauri Wizara juu ya uendeshaji wa Wakala, kusimamia na kushauri juu ya maslahi ya wafanyakazi, kufanya tathmini ya utendaji kazi wa Wakala, kuweka vipaumbele na malengo yatakayotekelezwa na Wakala.
Ameongeza kuwa kuzinduliwa kwa Bodi hiyo kunakamilisha uundwaji wa uongozi wa ADEM baada ya kukamilika kwa mchakato wa uteuzi wa Mtendaji Mkuu ambaye ni Dkt. Mauli Jumanne Maulid.
Bodi mpya inaundwa naDkt. Leonard Douglas Akwilapo - Mwenyekiti, Katibu Mkuu Mstaafu, Wizara ya Elimu, Sayansi naTeknolojia, Bw. Mwanyika Semroki - Kaimu Mkaguzi Mkuu wa Ndani kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Jane Simon Kaji -Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Miundo ya Wakala za Serikali - Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Coletha Luoga Komba - Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe.
Wengine ni Dkt. Joel Jonathan Kayombo - Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE),Bw. Abdul Maulid Mnonya - Mkurugenzi wa ElimuMsingikutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, na Bi. Susana Saverina Nussu - Mkurugenzi MsaidiziSekondari kutoka Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).