Imeandikwa na Dira Makini
15 Juni,2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amepokea Taarifa ya Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Balozi Ombeni Sefue.
Hafla ya upokeaji imefanyika Juni 15, 2024 Ikulu Chamwino jijini Dodoma wakati wa hafla ya kukabidhi Taarifa ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai kwa Rais Dkt. Samia.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu, Mhe. Balozi Ombeni Sefue ameyasema amemweleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa, Jeshi la Magereza nchini lipo katika mazungumzo na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), VETA na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi ( FDC ) ili kutoa mafunzo kwa wafungwa kwa kuzingatia Mitaala iliyopo.
Amesema, elimu hiyo itawasaidia wafungwa wanapotoka magerezani kuwa na vyeti na ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko.
"Vile vile Jeshi la Magereza limeanza mazungumzo na taasisi kama vile Chuo Kikuu Huria, VETA na FDC ili kuwisanisha mitaala inayotolewa Magerezani na ile itolewayo uraiani ili iwe rahisi kwa wafungwa wanaomaliza adhabu zao kurejea uraiani wakiwa na vyeti vinavyotambulika kulingana na elimu na ujuzi walioupata wakiwa Magerezani."