Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imekutana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kujadili utekelezaji wa majukumu ya Elimu ya Ualimu na maendeleo ya elimu ya ufundi na mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ambapo kamati hiyo imeridhishwa na utekelezaji na mipango ya kuimarisha ngazi hizo za Elimu.
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Husna Sekiboko huku Menejimenti ya Wizara na VETA wakiongozwa na Mhe. Omari Kipanga Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.