Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Agosti 13, 2024 ameshiriki Programu ya Ushirikiano wa Mabadilishano katika Mageuzi ya Elimu kwa nchi za Jumuiya ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) na Afrika Mashariki (EAC).



Program hii inalenga kuwezesha Nchi Wanachama wa ECOWAS na EAC kutekeleza mahusiano katika Elimu Msingi, Ubora wa Usawa unaojumuisha Jinsia na Elimu ya Kidigitali.



Programu hii imefanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC Jijini Arusha.