Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amepongeza jitihada zinazofanywa na Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) katika kazi ya kusimamia Vyuo vya Ufundi nchini.
Dkt. Rwezimula ameyasema hayo leo Agosti 30, 2023 alipotembelea ofisi za NACTVET Jijini Dar es Salaam na kukutana na Uongozi na Watumishi wa Taasisi hiyo na kupewa taarifa fupi ya utendaji kazi iliyotolewa na Katibu Mtendaji Dkt. Adolf B. Rutayuga.
Aidha Dkt. Rwezimula ameongeza kuwa bado kuna kazi ya kuongeza idadi ya wanafunzi wanaojiunga na vyuo hivyo ili kuongeza vijana wenye ujuzi ambao utawawezesha kujiajiri au kuajiriwa pindi wanapomaliza mafunzo na kupunguza tatizo la ajira nchini.
Pia amewaasa wasiachwe nyuma na maendeleo ya TEHEMA kwa kuwa itawafikia wadau wengi na kuongeza uelewa juu ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa NACTEVET amesema wameanza jitihada mbalimbali za kuongeza uelewa kwa umma juu ya Baraza hilo na kutoa elimu Juu ya majukumu ya Baraza pamoja na taratibu za udahili wa wanafunzi katika vyuo vya Ufundi.