Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Septemba 26, 2024 imekabidhi nakala ya Vitabu vya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 kwa Viongozi wa Kisiasa Wanawake Tanzania.
Makabidhiano hayo yamefanywa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda na Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo Mkoani Ruvuma wakati wa Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa kwa Viongozi hao yaliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT).
Vitabu hivyo vimepokelewa na Mwenyekiti wa UWT Mary Chatanda Mary Chatanda ambaye ameahidi kuisemia Sera hiyo katika makundi mbalimbali ili watanzania waielewe na kuifahamu