Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Hamis Nderiananga amesema Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga na kukarabati miundombinu inayozingatia mahitaji maalum ya wanafunzi kuanzia elimu ya awali mpaka vyuo vikuu



Ameyasema hayo leo Disemba 5 2024 Mkoani Morogoro kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya kuwajengea uelewa Mawaden 147 kutoka kwenye Taasisi za Elimu ya juu zinazopokea Wanafunzi wenye mahitaji Maalum



Mhe Nderiananga amesema Serikali imeandaa na kusambaza miongozi ya kitaifa ya utoaji wa elimu maalumu na elimu jumuishi katika ngazi zote za elimu ikiwemo mwongozo wa shule ya nyumbani na mwongozo wa ubainishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum



"Serikali imenunua na usambazaji wa vifaa vya kielimu na teknolojia saidizi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kuanzia elimu ya awali mpaka Elimu ya juu vikiwemo Laptops, Tablets, Digital Voice recorder, bajiji, shime sikio, viti mwendo, embosser machine na fimbo nyeupe, Obite Reader"



Ameongeza kuwa Serikali imetooa ufadhili unaoitwa Samia Scholarship kwa wanafuzi wenye mahitaji maalum 32 waliofaulu kwa kiwango cha juu katika masomo ya Sayansi, Teknolojia na Hisabati kwa lengo la kuhamasisha usomaji wa masomo hayo na kuongeza fursa kwa wote.



Kwa upande wake Mkurugenzi wa Elimu Maalum kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Margret Matonya amesema Lengo la mafunzo haya ni kuhakikisha kuwa Mawaden wanapata stadi na maarifa ya namna ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji Maalum na kuwasaidia kutimiza ndoto zao