Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknoljia Prof. Carolyne Nombo alikutana na Mkuu wa Ushirikiano katika Masuala ya Elimu kutoka Serikali ya Canada Bi Hellen Fytche aliyefika Ofisini kwake kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini.
Mkutano huo umefanyika Juni 27, 2024 Jijini Dar es Salaam ambapo Katibu Mkuu alimshukuru Bi Fytche kwa mchango wake katika sekta ya elimu hasusan katika kuimarisha Elimu ya Ualimu.
Kupitia miradi mikubwa miwili iliyofadhiliwa na Serikali ya Canada Teacher Education Support Project ( TESP) na Upgrading Teachers Colleges (UTC) vyuo vya ualimu vya Serikali takriba kumi na tatu (13) vimekarabatiwa na vingine kujengwa upya ikiwemo Chuo cha Ualimu Kabanga, Mpuguso, Ndala, Shinyanga na Kitangali na kuleta matokeo chanya kwa walimu tarajali katika ujifunzaji pamoja na kuongeza fursa za masomo.
Bi. Fytche alimshukuru Katibu Mkuu na wasimamizi wa miradi ambao amefanya nao kazi kwa ushirikiano na kwamba pamoja na yeye kuondoka Serikali ya Canada itaendelea kusaidia katika kuhakikisha utekelezaji wa mageuzi ya elimu unakuwa na mafanikio.