NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Daniel Mushi amewataka waratibu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET),kuongeza kasi ya mchakato wa manunuzi pamoja na kusimamia fedha kwa weledi,ili zifanye kazi iliyo kusudiwa.
Ameyasema hayo leo Oktoba 10,2024 Jijini Dar es salaam wakati alipokutana na waratibu hao kwa lengo la kutathnimi utekelezaji na kuweka mikakati ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huo ili ukamilike kwa wakati.
Amesema mradi huo unaouhusisha taasisi 22 za elimu ya juu pamoja na elimu kati ambapo zimetengewa fedha zaidi ya shilingi billion 900 za kitanzania kutokana na mkopo nafuu wa Benki ya Dunia ukiwa na lengo la kuuongeza fursa za elimu ya juu nchini na kuimarisha mafunzo na ujifunzaji.
Aidha Naibu Katibu Mkuu huyo amesema kukutana huko kwa waratibu ni maandalizi kabla ya kupokea ugeni kutoka Benki ya Dunia makao makuu ambao watakuja kwa ajili ya kufanya tathimini ya kati ya Maendeleo ya mradi.
Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi umekusudia kuboresha mazingira ya kujifunzia pamoja na kufundishia ili wahitimu watakaopatikana kupitia vyuo nufaika waweze kukidhi mahitaji ya soko la ajira wanapoajiriwa au kujiajiri na hivyo kuchangia katika uchumi wa nchi