Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) pamoja na kazi ya ujenzi ili kuongeza fursa za mafunzo ya elimu ya juu lakini pia kutoa mafunzo na kuweka mifumo ikiwemo kuwa Sera ya Jinsia (Gender Policy) na kuunda Dawati la Jinsia (Gender Desk) katika Vyuo.



Leo Juni 29, 2024 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omary Kipanga amefungua Mafunzo ya kuwajengea uwezo Menejimenti ya Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) katika masuala ya Jinsia na matumizi ya mfumo wa Serikali wa e - Mrejesho wa kutuma na kupokea malalamiko.



Akizungumza katika ufunguzi huo Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Qs Omary Kipanga amesema kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha afya na ustawi wa akili ili kufikia malengo.



Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Prof. Maulilio Kipanyula ameeleza kuwa, mafunzo hayo ni utekelezaji wa matakwa ya mradi wa HEET ya kuwafundisha washiriki kutambua na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum, afya ya akili, jinsia, ukatili na unyanyasaji wa kijinsia ili kutoa huduma bora kwa wadau.