Leo Septemba 4, 2023 jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amekutana na kufanya mazungumzo na Wadau wa Elimu Henry Kulaya na Diana Ninsiima ambao wamewasilisha suluhisho la kufundishia kwa kutumia mifumo ya TEHAMA ( Virtual Reality) itakayosaidia kurahisisha utoaji elimu kwenye Vyuo vya Maendeleo ya Wanachi ( FDC's) na Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
Wadau hao wamewasilisha suluhisho hilo kwa Katibu Mkuu na wataalamu katika eneo hilo ili kwa pamoja kujadili na kuona kama suluhisho hilo litavyowezesha utoaji wa elimu katika kipindi hiki ambacho kuna mageuzi ya elimu na kuweka utaratibu na mpango wa utekekezaji.
Kikao hicho kimehudhuriwa na wataalamu kutoka Wizarani na VETA