Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Charles Mahera anashiriki mkutano wa Kimataifa wa Lishe ya Mtoto unaofanyika jijini Osaka nchini Japan.
Mkutano huo umewakutanisha viongozi na washirika mbalimbali kubadilishana uzoefu juu ya program mbalimbali za chakula na lishe kwa watoto shuleni.