Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda (kulia) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-Maamry Mwamba (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Atupele Mwambene.

Viongozi hawa wamekutana Disemba 2, 2023 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa GPE Laura Frigenti kuzungumzia masuala muhimu katika sekta ya elimu nchini Tanzania kuelekea kuanza kwa mkutano wa Bodi ya Shirika hilo Jumatatu Disemba 5, 2023 visiwani Zanzibar.