Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Daniel Mushi, amesema kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) katika kuboresha miundombinu na kuhakikisha mitaala yake inaendana na mahitaji ya soko la ajira.
“Nimeridhishwa na juhudi za chuo katika kuongeza udahili na programu mpya zinazoendana na mahitaji ya viwanda. Serikali itaendelea kuwa mshirika wa karibu katika juhudi hizi,” amesema Prof, Mushi.
Akihitimisha hotuba yake, Prof. Mushi amewataka wahitimu kuwa mabalozi wa Chuo cha Ufundi Arusha ndani na nje ya nchi.
“Sifa na umaarufu wa chuo hiki zinategemea jinsi mtakavyojionesha katika kufanya kazi kwa bidii na kutumia ujuzi wenu kikamilifu” alihitimisha Prof. Mushi.
Prof. Mushi ameeleza hayo Disemba 05, 2024 Jijini Arusha akizungumza katika mahafali ya 16 ya chuo hicho