Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga leo Desemba 19, 2023 amefika Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Arumeru na Kukutana Mkuu wa Wilaya hiyo Emanuela Kaganda kabla ya kuelekea Kukagua Shughuli za ujenzi wa VETA ya Wilayani hiyo.
Pia Naibu Waziri huyo alipata wasaa wa kusikiliza na kujibu hoja za baadhi ya wananchi waliofika kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Arumeru kuhusu sekta ya elimu.