Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) Bi. Bernadetta Ndunguru ambae alifika kwa ajili ya kujitambusha .
Katika kikao hicho Prof. Mkenda amesisitiza Bodi ya NACTVET kuendelea kuimarisha na kusimamia elimu ya Ufundi katika kutekeleza Sera ya Elimu na Mafunzo inayojielekeza katika elimu ujuzi.
Nae Bi. Bernadetta Ndunguru amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu kwa kuaminiwa katika nafasi hiyo pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kuahidi kutekeleza jukumu la kusimamia na kuendeleza Elimu ya Ufundi na mafunzo ya ufundi Stadi kwa ufanisi.
Ameongeza kuwa anafahamu vilio vya ajira nchini, hivyo jukumu moja wapo ni kuhakikisha mafunzo yanayotolewa yanawezesha wahitimu kupata maarifa na ujuzi utakaowawezesha kujiajiri au kuajirika ndani na nje ya nchi.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri Mhe. Omar Kipanga na Naibu Makatibu Wakuu Prof. Daniel Mushi na Dkt Wilson Mahera