Naibu katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Rwezimula amewataka wasimamizi wa ujenzi wa chuo cha VETA kigamboni kuongeza kasi ya ujenzi ili ukamilike kwa wakati uliopangwa.

Ameyasema hayo August 28 alipotembelea eneo la ujenzi wa chuo hicho kigamboni jijini Dar es salaam na kujionea hatua za awali za ujenzi wa chuo hicho.

Amefurahishwa kukuta baadhi ya wanafunzi wa chuo hicho wakifanya mafunzo kwa vitendo kupitia shughuli mbalimbali za ujenzi zinazoendelea