Karibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Mei 17 2024 amekutana na Balozi wa Poland Nchini Tanzania Mhe. Krzystof Buzalski ambapo wamezungumzia kuhusu kuendelea kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta ya Elimu.



Katibu Mkuu Nombo amemueleza Balozi huyo kuwa Tanzania inafanya mageuzi makubwa katika sektacya elimu ikiwemo kutilia mkazo elimu ya Amali inayolenga kujenga ujuzi kwa Vijana ili washiriki kikamilifu katika maendeleo kupitia nyanja mbalimbali za uzalishaji.



Prof. Nombo ameiomba Poland kushiriki kwa namna mbalimbali katika kutekeleza mageuzi hayo kwani yanahitaji rasilimali za kutosha ikiwemo fedha na wataalam katika eneo la kiufundi ili kufikia malengo yanayotarajiwa.



Mhe. Buzalski ameipongeza Serikali ya Tanzania Kwa kuboresha miundombinu mbalimbali ya Elimu na kuanza utekelezaji wa Sera na Mitaala mipya ya Elimu na kuahidi kutoa ushirikiano katika utekelezaji.