Mratibu wa Masula ya Lishe Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Abigail Marwa ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuwa miongoni mwa Wizara mtambuka zinazochangia na kusimamia kikamilifu suala la chakula na lishe Shuleni.
Mratibu huyo amesema hayo Julai 25, 2024 Jijini Dodoma wakati akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Utoaji Chakula na Lishe Shuleni, ambapo amesisitiza kuwa kama Taifa tuna jukumu la kushirikiana kuhakikisha tunaweka mkazo na kuhamasisha huduma ya chakula na lishe Shuleni, hatua itakayosaidia kukabiliana na changamoto ya udumavu kwa watoto na kuwezesha afya bora na ujifunzaji mahiri.