Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, amepanda Mti wa Kumbukumbu katika Chuo cha Ualimu Dakawa, mkoani Morogoro. Tukio hili limefanyika sambamba na uwekaji wa jiwe la msingi la majengo mapya ya chuo hicho, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.