Mwenyekiti wa Kamati ya kukusanya maoni kwa ajili ya kufanya mapitio ya Sheria ya Elimu Prof. Eustella Bhalalusesa amesema wadau wana mchango mkubwa kwa katika zoezi hilo muhimu kwa taifa, hivyo wana jukumu la kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni kuhusiana na changamoto zilizopo kwenye Sheria ya Elimu Sura ya 353.



Prof. Eustella amesema hayo Oktoba 31, 2024 jijini Dar es Salaam akizungumza baada ya kikao na wadau wa maendeleo akisisitiza kuwa, Serikali ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa Sera ya Sera ya elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023, kuna matamko mbalimbali ambayo yanatakiwa kufanyiwa kazi ili yaingie kwenye sheria ya elimu, kwa pamoja viweze kwenda sambamba kuwezesha ufanisi katika kutekeleza Sera hiyo.



Nae Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Adv. Innocent Mgeta amesema kamati hiyo inaendelea na vikao vyake kushirikisha wadau mbalimbali kufanya mapitio ya Sheria ya Elimu kuwezesha ufanisi katika utekelezaji wake.



kwa upande wake Mshauri wa Elimu kutoka Ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania Dkt. John Lusingu amesema, kikao hicho kimewapatia nafasi ya kufahamu masuala mengi ikiwemo muundo wa elimu na majukumu mbalimbali ya Serikali katika kuendeleza, na kwamba ni jambo kubwa makundi hayo kutoa maoni juu ya sheria ya elimu kwani ndio roho ya sekta hiyo