Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akiwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe kuona maendeleo ya utoaji Elimu na utekelezaji wa Mitaala iliyoboreshwa.



Shule hiyo kongwe iliyoanza Mwaka 1965 ni miongoni mwa Shule zinazotoa Mafunzo ya Amali, ina mchepuo wa Kilimo, Ushoni na Mapishi.