#Ni katika kuimarisha kazi ya usimamizi na ufuatiliaji

Uwepo wa vitendea kazi ikiwemo magari ni muhimu katika kuwezesha kutekeleza kazi za kuimarisha utoaji elimu bora Nchini.

Leo tarehe 16, Novemba 2023, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amepokea magari mawili yaliyotolewa kupitia mradi wa "Shule Bora" unaofadhiliwa na UK Aid.



Akipokea msaada huo Dkt.Rwezimula amesema mradi unatekeleza kazi mbalimbali katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha Sekta ya Elimu nchini.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Taasisi Elimu Tanzania TET, Jijini Dar es Salaam