Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Husna Sekiboko imeendelea na vikao vya Kupitia taarifa za Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara na Taasisi zake.
Leo ilikua ni zamu ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ambapo imewasilisha taarifa ya Utendaji ya Bodi kwa Mwaka wa fedha 2023/24.
Katika kikao hicho Wizara iliongozwa na Waziri wa Elimu. Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ambae alitumia nafasi hiyo kupongeza Kamati hiyo kwa kazi kubwa inayofanya kuhimiza uwezeshaji utoaji mikopo kwa Wanafunzi.