
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Adolf Mkenda, amewasili Brazzaville, Jamhuri ya Congo, na kupokelewa na Balozi wa JMT nchini humo mwenye makazi yake Kinshasa Baloz Juma Said Mshana

Waziri Mkenda anamwakilisha Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa JMT katika Sherehe ya Uapisho wa Rais wa Jamhuri ya Congo zinazotarajiwa kufanyika tarehe 16, Aprili, 2026 Jijini Brazaville


