Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda tayari amewasili wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma katika eneo kinapojengwa Chuo cha Ufundi Stadi VETA, ambapo leo Agosti 20, 2024 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Philip Mpango atatembelea eneo hilo kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo hicho.