Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga yupo Abu Dhabi, Falme za Kiarabu kwa lengo la kushiriki Mkutano wa UNESCO kuhusu Elimu ya Utamaduni na Sanaa.
Mkutano huo wa siku tatu ulioanza tarehe 13 hadi 15 Februari 2024, utatoa fursa kwa wajumbe kutoka nchi wanachama kupitishwa katika Kiunzi cha Elimu ya Utamaduni na Sanaa ( Framework for Culture and Arts Education).
Pia wajumbe watapata nafasi ya kutoa uzoefu wa nchi zao katika eneo hilo la Elimu ya Utamaduni na Sanaa.
Siku ya kwanza ya mkutano Mhe. Kipanga alipata nafasi ya kutoa mchango wa nchi ambapo pamoja na masuala mengine alieleza jinsi Tanzania inavyotoa msukumo katika Elimu ya Utamaduni na Sanaa hasa kufuatia mabadiliko ya Sera na Mitaala ya Elimu.
Pia Naibu Waziri alisema, ili kufikia azma ya upatikanaji wa elimu bora kwa wote ni muhimu kuendelea kuwekeza katika digital technology. Hivyo aliiomba UNESCO kuzisaidia nchi zinazoendelea katika eneo hili ili ziweze kupiga hatua.