Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo Leo Agosti 21, 2023 Jijini Dodoma, amekutana na watumishi wa Idara na vitengo zilivyo chini ya Ofisi ya  Kamishna wa Elimu.

Kikao hicho chenye lengo la kuweka mikakati ya pamoja ya kuhudumia kwa ufanisi wadau wa elimu  wanaohitaji huduma mbambili kutoka katika ofisi hizo.

Prof. Nombo  amewataka watumishi hao kusimamia na kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuongeza kasi ya kuwahudumia wadau wanaofika katika ofisi hizo kwa wakati.