
Waziri wa Ujenzi Mhe Abdallah Ulega akizungumza kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Philip Mpango katika hafla ya Tuzo za Mwalimu Nyerere za Uandishi Bunifu jijini dar es Salaam.
Ulega amepongeza Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kuanzisha TUZO ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo inakuza lugha na kuongeza kuongeza hifadhi ya Vitabu vya fasihi vya kiswahili pamoja na kuibua na kukiza vipaji vya watanzania Waandishi Bunifu.