Uwepo wa bidhaa bunifu na endelevu za masoko ya mitaji ikiwemo utoaji wa hatifungani za kugharamia na kuendeleza miradi ya maendeleo imefungua milango kwa Mataifa mbalimbali kuja Tanzania kupata ujuzi wa namna ya kutekeleza mikakati inayochangia maendeleo ya masoko ya mitaji kwenye Mataifa yao.



Hayo yamebainishwa Februari 28, 2024 wakati Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akifungua mkutano wa siku tatu kuhusu maendeleo ya masoko ya mitaji katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Dkt Mwigulu Nchemba.