Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi ametembelea na kuzindua majaribio ya mfumo wa ufundishaji mubashara "Live Teaching" ambao utawezesha wanafunzi wa shule mbalimbali nchini kuunganishwa na mwalimu anayefundisha katika shule ya Sekondari Kibaha ili kukabiliana na changamoto ya uhaba walimu nchini.



Mfumo huo ni moja ya mipango ya Serikali ya kutumia TEHAMA katika ufundishaji ili kutatua Changamoto ya upungufu wa walimu.

Uzinduzi wa majaribio hayo umehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula ambae amesema kupitia Kampuni ya Edutech ya China ilitoa seti tatu za vifaa kuwezesha Smart classrooms.



Vifaa hivyo vimetolewa kwa Taasisi ya Elimu Tanzania ambapo itatumika kutoa mafunzo kwa walimu kazini, Shirika la Elimu Kibaha pamoja na Zanzibar.

Majaribio yamefanyika kupitia vifaa vilivyotolewa kwa Shirika la Elimu Kibaha ambapo wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dodoma waliunganishwa na mwalimu anayefundisha akiwa Kibaha Sekondari.



Baada ya majaribio ya leo katika Shule ya Sekondari Dodoma mfumo utaenda katika Shule 10 na baadaye utasambazwa katika Shule zote nchini