Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akishuhudia maoenesho katika Kongamano la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Agosti 25, 2025 JNICC jijini Dar es Salaam.



Kongamano hili linatoa msukumo wa kitaifa katika kuimarisha sera na mikakati ya elimu endelevu, hasa kwa makundi yaliyo pembezoni mwa mfumo rasmi wa elimu na kujadili mafanikio, changamoto, na fursa za kuboresha elimu ya watu wazima nchini.