Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo mapema leo atembelea Viwanja vya Satellite City Nkokoto A, kukagua maandalizi ya uwekaji jiwe la msingi la Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi Veta Wilaya ya Igunga mkoani Tabora.



Prof. Nombo ametumia fursa hiyo kuteta masuala kadhaa na menejimenti ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) juu ya umuhimu wa tukio hilo katika mstakabali wa upatikanaji wa mafunzo na ujuzi kwa vijana wa Kitanzania kuwawezasha kujiajiri na kuajiriwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa chuo hicho.