#Ujenzi wafikia 96%
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Dodoma City inayojengwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia maarufu kama Shule ya Mfano, Jijini. Dodoma.
Akizungumza Januari 09, 2024 baada ya kukagua ujenzi huo, Prof. Mkenda amesema kwa hatua iliyofikia na kwamba Wizara iko tayari kwa uzinduzi kabla yavkuikabidhi Ofisi ya Rais Tamisemi.
Mkenda amesisitiza kuwa uendeshaji wa shule hiyo uzingatie Sera na Mitaala mpya ambapo ametaka kuweka msisitizo katika masomo ya sayansi na kuzingatia uwepo wa mafunzo ya Amali.
Mkenda amepongeza Mkandarasi wa mradi huo (SUMA JKT) kwa kufanya kazi nzuri na kwa ubunifu, na hasa kutengeneza mfumo wa maji taka utakao wezesha kuzalisha gesi kwa kutoa maji kwa ajili ya unwagiliaji ambapo hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa Shule.
Mkurugenzi wa SUMA JKT Kanali Petro Mgata ameahidi kukamilisha shughuli zote zilizosalia ndani ya mwezi mmoja na kukabidhi Shule hiyo.
Kwa upande wake Meya wa Manispaa ya Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe amesema uwepo wa Miundombinu ya viwango katika Shule hiyo ya Mfano ni kielelezo tosha kuonesha utashi wa serikali katika kuendelea kuimarisha miundombinu na kutoa Elimu bora kwa watoto wa Kitanzania, ili waweze kuchangia maendeleo ya Taifa lao na jamii lakini.
"Shule ni kivutio cha kujivunia hapa Dodoma na ninkielelezo dhahiri cha utashi wa Serikali ya Awamu ya Sita katika kujenga miundombinu bora ya Elimu" alibainisha Prof. Mwamfupe.
Shule hiyo ya Mfano inajengwa na serikali ambapo ikikamilika itakuwa na uwezo wa kupokea Wanafunzi 1,000 na tayari imeanza kupokea wanafunzi wa Kidato cha Tano ikiwa na miundombinu yote stahiki.