Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo, amesema Mafunzo kwa walimu kuhusu utekelezaji wa Mtaala ulioboreshwa ni endelevu na yanalenga kuwezesha Walimu wote Nchini kufundisha kwa umahiri.



Katibu Mkuu huyo ameeleza hayo alipotembelea Shule ya Msingi ya Prince & Princess iliyopo Jijini Tanga kuangalia namna Shule hiyo inavyotekeleza Mtaala Mpya ulioboreshwa, ambapo amesema Serikali inatambua mchango wa sekta Binafsi katika kutoka Elimu hivyo itaendelea kushirikiana kikamilifu katika kutekeleza azma ya mageuzi ya Elimu.



"Serikali inaweka mazingira mazuri kuwezesha sekta Binafsi kushiriki kikamilifu katika kutoa elimu, nasisitiza ziendelee kufuata kanuni, taratibu na sheria zote na kuzingatia mwelekeo wa sasa wa Elimu ya Amali.



Aidha, amekoshwa na Shule hiyo kuanza utekelezaji wa Mtaala ulioboreshwa na kwamba hatua hiyo ni chachu kwa Tanzania kuelekea mageuzi katika Elimu huku akisisitiza Walimu kufundisha masomo yote kwa ufanisi ikiwemo lugha ya Kingereza na Kiswahili pamoja na somo la Tanzania na Maadili.



Nae Damas Kifanga Mkuu wa Shule ya Msingi Prince and Princess ameishukuru Serikali kuwapatia mafunzo Walimu wa Shule hiyo na kwamba yamewezasha kutekeleza Mtaala Mpya.



"Ni vizuri Wazazi na jamii wakaelimishwa vya kutosha, hasa kuhusu dhana ya mkondo wa amali, ili waweze kushiriki katika kushauri watoto kwa kuzingatia vipawa walivonavyo.