Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuzindua Mfuko wa Mikopo wa kusaidia Ubidhaishaji na Ubiasharishaji wa ubunifu na teknolojia zinazobuniwa na vijana wa Kitanzania.
Akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari Novemba 6, 2024 Jijini Dodoma akielezea kuwapo kwa Kongamano la Tisa la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kongamano hilo linatarajia kufanyika kuanzia Disemba 2 hadi 4, 2024.
Prof. Mkenda amesema kuwa mfuko huo unaanza kiasi cha shilingi bilioni 2.3 ambazo zitatumika kukopesha wabunifu kuendeleza kazi zao.
Aidha, Waziri Mkenda amesema kuwa mbali na uzinguzi wa mfuko huo, Mhe. Rais atakabidhi hundi yenye thamani ya bilioni 6.3 kwa watafiti 16 ambao tafiti zao katika masuala ya mabadiliko ya tabia Nchi.
Mhe. Rais pia anatarajiwa kuwatambua na kutoa tuzo kwa wanasayansi na wabunifu ambao Matokeo ya kazi zao zimechangia kuleta maendeleo ya Kiuchumi na kijamii ndani na nje ya nchi.