Mhe. Prof. Adolf Mkenda Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia amemwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Isdor Mpango katika Hafla ya Uzinduzi wa Majengo ya awali katika Shule ya Shirika la Masista wa Maria Boystown iliyopo Kikombo Halmashauri ya wilaya ya Jiji la Dodoma
Waziri Mkenda aishukuru kanisa la katoliki kwa kuwa miongoni mwa mashirika yanayoleta chachu yakuendeleza mageuzi ya Elimu nchini ikiwemo kuendelea kutambua dhamira ya Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujenga miundombinu wezeshi ya elimu kwa wanafunzi hao.
Waziri wa elimu amefurahishwa zaidi kwa lengo moja wapo la uanzilishi wa Shule ya masista hii nikuwapatia watoto elimu wenye hali ya chini ili watakapo elimika ili wanaporudi katika jamii zao husika wapate kuendelea kimaarifa na kuwa chachu ya kutokomeza umaskini huku Waziri huyo akiahidi kufika Shule ya Wasichana Girls town iliyopo Kisarawe na kuwa miongoni mwa watu watakao weka nguvu na aariii katika Ujenzi wa barabara kuu kuelekea katika Shule hiyo.
Mhe. Rosemary Senyamule Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amewaasa Masista wa Maria kuendeleza juhudi za kuwainua wanafunzi waliopo katika mazingira magumu na kuwawezesha kupata elimu kwani Mkoa wake takwimu zinaonyesha kuna kundi kubwa la wahitaji hivyo kuhakikisha wanasadia ili kuondokana na kundi hili tegemezi Jijini Dodoma. Pia ametumia jukwaa hilo kuwakaribisha wageni wote waliotoka nje ya Dodoma na nje ya nchi Kufanya uwekezaji mkubwa zaidi katika makao Makuu ya nchi.
Aidha, kwa upande wa Mkuu wa Shule ya shirika la Maria sista Elena Belarmino amesema Shirika la Masista wa Maria kwa sasa ina vijana 110 kutoka Mkoa mbalimbali ndani ya nchi wenye mazingira magumu hivyo amewaomba wavulana hao kutoa hofu kwani wameanza kusoma Shule hiyo wakiwa na umeme, mazingira mazuri yakusoma kwa amani huku wakilelewa kiroho na kimaadili. Mkuu wa shule hiyo ameseama wanatarajia kupokea wanafunzi wengine wapatao 50 kufikia mwsho wa mwaka 2023.
Sista Elena Belarmino ameongezea kwakusema punde shule hiyo ikikamilika Itakua na uwezo wakuchukua zaidi a watoto elfu moja Shirika la Masista wa Maria lina jukumu la kuwapatia elimu bora vijana kwa uweledi na itakaygusa kila Nyanja yakumuelemisha mwanafunzi na sio kutegemea elimu ya darasani tu ila itagusa hadi elimu ya ujuzi na msingi mzuri wa tabia na maadili yaliyo bora na kuwahimiza wanafunzi kuangalia na kutunza vitendea kazi kwa manufaa yao na ya wadogo zao watakao kuja shuleni hapa.