#kuhakikisha zinatumika kutatua changamoto za kijamii

Serikali itaendelea kutekeleza mikakati ya kuhakikisha Bunifu zinazozalishwa nchini na zinaingia sokoni pamoja na matokeo ya tafiti za wanasayansi kutumika ili kutatatua changamoto za mbalimbali za kijamii.



Akizungumza Disemba 04, 2024 wakati wa kufunga Kongamano na Maonesho ya Tisa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa mfuko wa kuwasaidia wabunifu umetoa zaidi ya shilingi bilioni 6 kuwezesha wabunifu kuingiza bidhaa sokoni.



Aidha Prof. Mkenda amewataka watafiti waliopata fedha kwa ajili ya kufanya utafiti juu ya tabianchi kuhakikisha tafiti hizo zinanufaisha nchi ikiwemo kuongeza tija katika kilimo katika maeneo ambayo yamekuwa yakisumbua na kuhakikisha tafiti zinakidhi matakwa ya ajenda ya kimataifa ya mabadiliko ya tabianchi.



Ameongeza kuwa ili nchi iwe na maendeleo inahitaji kuwa na rasilimaliwatu bora yenye maarifa na ujuzi elimu inayohusha pia maarifa na ujuzi katika sayansi, teknolojia, ubunifu ambao watakuwa na uwezo wa kuchakata rasilimali asilia za nchi na kuwa na kuchagiza maendeleo endelevu yanayotokana na mtaji wa rasilimaliwatu hiyo.



Kiongozi huyo amesema ili kuwa na maendeleo endelevu ni lazima kuongeza uwekezaji katika elimu hasa katika maeneo ya sayansi na teknolojia kwa kuimarisha matokeo ya ubunifu na ujuzi, hivyo Serikali itaendelea kuhakikisha inasaidia vijana wanaosoma sayansi kwa kuendelea kutoa mikopo bila kuchoka na kuchagiza tafiti.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Utamaduni, Michezo na Sanaa Mhe. Husna Sekiboko ameipongeza serikali kwa kuanzisha mfuko wa kuwasaidia wabunifu na kuahidi kuweka msukumo kuhakikisha mfuko huo unaongezewa fedha ili kuwezesha bunifu na tafiti zinakwenda kuleta tija katika taifa