Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Flanklin Rwezimula Amefurahishwa na hatua za Ujenzi wa VETA Misenyi na kuhimiza Ushirikiano kati ya Wasimamizi wa Mradi na Serikali ya wilaya ya Misenyi katika kutatua changamoto zitakazo Jitokeza katika hatua mbalimbali za ujenzi wa Mradi.


Ametoa rai hiyo September 13, 2023 Alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Chuo hicho na kukutana na wasimamizi wa Mradi na kuona hatua za awali za Ujenzi zinavyoendelea.


Chuo cha VETA Misenyi ni kati ya vyuo 64 vinavyoendelea kujengwa nchini ili kukamilisha azma ya Wilaya zote nchini kuwa na Vyuo vya VETA vya Wilaya na kila Mkoa kuwa na Chuo cha VETA Mkoa.