Mkurungezi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amewataka waandishi wa vitabu nchini kuviwasilisha TET ili vipatiwe ithibati kwa ajili ya kutumika shule.
Dkt. Komba amesema hayo Agosti 02, 2024 Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Kitabu cha Mwandishi Euanice Urio kiitwacho *Tangled Web* ambapo amesema utaratibu wa kupeleka vitabu TET ni wa kawaida ili kuona kama vina maudhui yanayoweza kutumika shuleni na kuwajenga watanzania.
Dkt. Komba ameongeza kuwa vitabu vya riwaya vya Kiingereza na Kiswahili, hadithi za watoto na mashairi vinahitajika kwa wingi nchini na kwamba vitasaidia watoto wa kitanzania kusoma vitabu vilivyoandikwa na waandishi mahiri wa Tanzania.
" Katika mabadiliko ya mitaala imeanzisha ufundishaji na ujifunzaji wa masomo ya fasihi katika Kiswahili na Kiingereza kuanzia kidato cha tatu , hii ni nafasi kwa Waandishi kuandika vitabu vya kutosha ili kuwezesha watoto kutumia vitabu vilivyoandikwa na Waandishi Mahiri wa Tanzania" amesisitiza Dkt. Komba