Na WyEST
Dodoma
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknojia, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Uwekezaji wakutana pamoja kujadili namna ya kutatua changamoto ya upungufu wa Wanataaluma katika Vyuo Vikuu na Kati vinavyotoa Elimu ya Afya na Tiba nchini.
Kikao hicho kilichofanyika Januari 23, 2024 Jijini Dodoma kimeongozwa na Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe pia kimejadili changamoto ya miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika vyuo hivyo.
Katika majadiliano hayo Wizara hizo zimekubaliana kwa pamoja kufanya kazi kwa ukaribu ili kuzipatia ufumbuzi changamoto pamoja na kuboresha utoaji elimu katika vyuo hivyo
Kikao hicho pia kimehudhiriwa na wajumbe kutoka, TCU, NACTVET, Vyuo vya Elimu ya juu na kati vinavyotoa mafunzo ya afya na tiba